Connect with us

SWAHILI

MKATABA WA JOHO NA MUNG’ARO UTAFYONZA MALI KILIFI, AISHA AONYA

Published

on

Mwaniaji wa kiti cha Ugavana kaunti ya Kilifi, Aisha Jumwa, ameibua amadai ya kuwepo kwa njama za gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kufaidi nafasi za ajira Kilifi endapo Gideon Mung’aro atapita uchaguzi Jumanne Agosti 9, 2022.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Malindi ni kuwa endapo Mung’aro atapita Joho atanufaika na nafasi za kazi kaunti ya Kilifi akihoji kuwa hiyo ndio sababu kuu inayopelekea Joho kuendeleza kampeni za Azimio kwa ari eneo hilo.

Akizingumza katika misururu ya kampeni za muungano wa Kenya Kwanza eneo la Pwani, Jumwa amedai kuwa upo mkataba wa kufanikisha hilo kati ya Mung’aro na Joho.

“Gari zote anazotumia Mung’aro kwenye kampeni ni za gavana Joho na ndugu yake. Kuna mkataba ulipitishwa kati ya Mung’aro na Joho utakaofanya raslimali za kaunti hii ya Kilifi ziwe za Johona familia yake ndani ya miaka mitatu ikiwa Mung’aro atafaulu kuwa gavana. Nawasihi muwe macho na kukataa hilo,” Aisha alisema.

Hata hivyo kwa upande wake Gideon Mung’aro, amepinga madai hayo na kusema kuwa, Joho amekuwa akiendeleza kampeni za ODM kama kiongozi wa chama hicho eneo la Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari kaunti ya Kilifi Mung’aro amesema, “Huo ni upuzi tu. Mimi sina mkataba na mtu yeyote. Kwenye kampeni za 2017 Aisha alikuwa pamoja na Johona wakati mmoja nikataka kumleta rais ajenge barabara na huyo Aisha akanisuta na kuniambia napaswa kumheshimu Joho kisa ni kiongozi wa Pwani.”

Siku 15 pekee ndizo zimesalia kufikia uchaguzi mkuu na kura za maoni zinaonyesha kipute Kilifi ni cha farasinwawili; Mgombea wa chama cha  ODM Gideon Mung’aro na wa UDA Aisha Jumwa.

Mung’aro anatajwa kuongoza kura hizo Kwa asilimia 32 huku Aisha akifuata Kwa asilimia 21 huku asilimia 25 ya wanakilifi wakiwa hawajaamua watampigia nani kura.

Wakili George Kithi anashikilia nafasi ya tatu akiwa na asilimia 9 pekee.

Continue Reading
Advertisement
Comments

SWAHILI

MUNG’ARO HAKUSOMA KWENYE CHUO HIKI, CHUO ALICHOSOMEA MUNG’ARO CHASEMA

Published

on

By

Huku kura za uchaguzi mkuu zikikaribia, maswala mapya yanazidi kuibuka kila uchao la hivi punde kabisa likiwa swala masomo ya baadhi ya viongozi Pwani kupatikana na tashwishi.

Hii ni baada ya uhalisi wa shahada (digrii) kutoka kwa wagombea wa ugavana Mombasa; Ali Mbogo, Suleiman Shahbal, Abdulswamad Nassir, Hassan Omar na William Kingi kuonekana kuwa na dosari.

Sasa mamlaka ya Uhitimu wa Kitaifa ya Kenya (KNQA) yawageuzia bunduki wagombea wa ugavana wa Kilifi ikiwemo Aisha Jumwa na Gideon Maitha Mung’aro.

Tayari Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) kimejitenga kwa kutoa shahada kwa Gideon Mung’aro kupitia mawakili wa Ssebalu na Lule.

Chuo kikuu hicho kinasema cheti chochote alichonacho mtuhumiwa aliyetajwa kutoka chuo kikuu ni cha ajabu na hakuna cheti, stashahada au shahada iliyotolewa kwa anayedaiwa na hoja au nia yoyote ya kuvitumia ni kitendo cha udanganyifu.

Continue Reading

SWAHILI

JIMMY KAHINDI, MTETEZI WA WANYONGE

Published

on

By

Tukio ambalo wananchi wa eneo bunge la Magarini kamwe hawatolisahau, ni wakati alipomsaidia Mwakilishi wadi wao katika sakata ya kipande cha ardhi cha ekari 990 cha shamba la ADC katika maeneo ya Sabaki, Malindi ambapo wananchi wanyonge walikamatwa pamoja na kiongozi wao huyo (MCA) Edward Kazungu Dele wakidai haki yao ya ardhi.

Kupitia ukakamavu wa Spika wao ambaye ni wakili, Kazungu Dele na wanakijiji wake zaidi ya 40 kutoka Sabaki walitolewa korokoroni. Kiongozi huyu na watu wake walikuwa wakitetea haki yao kutoka jadi.

Hawa ni baadhi ya maskwota ambao wametoa kilio miaka nenda miaka rudi bila kilio chao kusikika .

Uchunguzi uliofanywa na Tume ya kupambana na ufisadi EACC ulibaini kwamba shamba hilo la ADC, lilinyakuliwa na hivyo lazima lirejeshwe kwa serikali ambayo iko chini ya wenye nchi (wananchi).

Utetezi wake umewahi pia kuwaokoa wengi hususan maeneo yenye shida kubwa ya unyakuzi wa ardhi na unyanyasaji katika eneo bunge la Kilifi Kusini. Ni hivi majuzi tu ambapo mwakilishi mwingine wa wadi ya Shimo la Tewa (Mtwapa), Said Ndago alishikwa na maafisa wa usalama waliotumiwa na bwenyenye mmoja ambaye alikuwa anawavunjia nyumba wanyonge mbele ya kiongozi wao.

Mwakilishi huyo na mamia ya wananchi wake walikamatwa na kupelekwa mahakamani ambapo kama kawaida yake Spika wa Kilifi, Jimmy Kahindi akisaidiana na seneta wa Stewart Madzayo na mbunge wa Kilifi Kusini, Ken Chonga alikuwa mstari wa mbele kutoa huduma zake za bure za uwakili.

Watu hushindwa kuelewa majukumu ambayo hupatiwa na mwananchi ama sekta fulani ya uongozi. Wengine hawajui kutofautisha kati ya bunge la kaunti na serikali ya kaunti.

Wanaomzungumzia katika kaunti hii, wanasema kuwa ari yake ya kusaidia wananchi wake kama kinara wa bunge la kaunti nzima imetokana na moyo wake wa kuhakikisha kwamba katika ulimwengu wa leo, hakuna mtu anayestahili kunyanyaswa na mwingine kwa sababu ya ukosefu wa uwezo fulani.

Jimmy Kahindi ana ajenda mahsusi ya kuiweka jamii ya Kilifi kwenye mseto sawa wa maendeleo na mipango maalumu ya mustakabali kwa wote kama, kutilia mkazo kilimo kwa uhakika wa upatikanaji wa chakula cha kutosha na pato la kibiashara.

Jimmy Kahindi anayo mikakati ya kuona kwamba jamii ya Kilifi imewekwa kwenye mazingira mazuri ya afya, kuweka miundo msingi thabiti ya kuonekana na umma na pia kuinua vipaji na uvumbuzi.

Jimmy Kahindi anafahamu fika umuhimu wa kuyalinda mazingira na faida ya uchumi wa masuala ya majini ambapo Kilifi inajivunia kuwepo kwa ufukwe wa bahari hindi. Uchumi huo utafungulia wengi fursa ya biashara za majini.

Jimmy Kahindi ana maono ya kuboresha maisha ya wana Kilifi kwa mipango maalumu ya ujenzi wa nyumba katika miji mikubwa ya Kilifi, miji midogo ama vituo vidogo vya biashara hadi vijijini ili kuweka usawa wa mazingira ya kuishi,kuinuahali ya michezo kwa vijana, kudumisha sanaa,turathi na utamaduni.

Katika kuhakikisha kwamba amekabiliana na suala sugu la ukosefu wa ajira kwa vijana, Jimmy Kahindi ana mpango mwafaka wa kuhakikisha kuwa uwekezaji wa viwanda zaidi Kilifi umepiga hatua na kudhibiti sekta ya huduma kwa wote huku ugavi wa kawi na mawasiliano ya kisasa kazingatiwa.

Jimmy Kahindi anafahamu umuhimu halisi wa utalii na sekta nzima hii inayojumuisha utamaduni na makavazi yetu Kilifi pamoja na mwamko mwengine wa masuala ya utalii. Upanuzi zaidi kwa miundo msingi chini ya serikali gatuzi ya Kilifi itapanuliwa na kutiliwa mkazo zaidi ili kutoa huduma inayoenda sambamba na pato la kiuchumi na kutoa nafasi ya kushuhudia faida ya pesa za umma na matumizi yake.

Continue Reading

Latest News

error: Content is protected !!
%d bloggers like this: